Tumeandaa na kupakua tamthilia mpya ya ‘Msiba Mziki’ kupitia Zuku Swahili Chaneli 100.
Tamthilia hii itaanza kurushwa kuanzia tarehe 1 Juni, 2026 saa moja na nusu usiku (1:30 Usiku), kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, na kurudiwa siku ya Jumapili kuanzia saa nane na nusu mchana (8:30 Mchana).
Muhtasari
Katika mtaa mmoja wenye majirani wa karibu lakini maisha tofauti, familia moja inakumbwa na simanzi kubwa baada ya kumpoteza mama yao mpendwa.
Wakiwa katika maandalizi ya msiba, machozi, majonzi na wageni wa pole vinatawala nyumbani kwao.
Upande wa pili wa nyumba, jirani yao yupo kwenye maandalizi makubwa ya sherehe ya harusi, muziki mkubwa, nderemo na furaha vikijaza anga. Kadri siku inavyoendelea, furaha
ya upande mmoja inaanza kugongana na huzuni ya upande mwingine.
Muziki mkubwa, wageni wenye shamrashamra, na maandalizi ya harusi vinazua migogoro, maneno makali, na vurugu kati ya majirani hawa wawili.
Kila upande unaamini uko sahihi, hali inayoufanya mtaa mzima kugawanyika.
Je, furaha inaweza kusimamishwa kwa ajili ya majonzi?
Au huzuni inaweza kuvumilia kelele za sherehe?
Msiba Mziki ni simulizi lenye vichekesho, drama, hekaheka na mafunzo kuhusu utu, ujirani, na umuhimu wa kuheshimu hisia za wengine.
Furahia tamthilia hii ya kusisimua kupitia Zuku Swahili chaneli 100.
Huduma ya Zuku Satellite TV inapatikana nchini kote.
Kama tayari umeunganishwa na mtandao wa Zuku Fiber, ongeza chaneli zaidi ya 100 za Premium (pamoja na filamu na tamthilia za Kiswahili, na tamthilia za Kiafrika) kwa Ksh 299 tu kwa mwezi, na ufurahie ligi za michezo za kitaifa na kimataifa ukiwa kwenye starehe ya sebule yako.
