Katika kijiji cha *NGAISA* Kilichopo kwenye jamii ya kimasai, “saitabau” kuna kijana ambae anatamani sikumoja watu wa jamii yake wabadilike na kuacha mila potofu zinazo leta ubaguzi katika jamii.
Katika mapambano yake atakutana na binti “NANJALA” (MANZI WA NAIROBI) Msichana mrembo kutoka Nairobi aliekuja Tanzania kwa niamba ya kupambania familia yake aliyo iacha uko Nairobi.
NANJALA Aliebeba jina la manzi wa Nairobi anafika namanga akiwa hana msaada. Simu yake ikiwa imepotea na akiwa hajui pakwenda. Saitabau ataamua kumsaidia bila ya kujua msaada huo utabadilisha kabisa maisha yake na kuleta vita kubwa katika familia yake.
SAMER Nikijana mwenye asili mbili yani umasai na mswahili. Samer akubaatika kuishi katika kabila la kimasai kwa upande wa mama yake. Aliishi uswahili na kubaatika kusoma adi kuwa mwanasheria wa ngazi ya wilaya. SAMER atajikuta akiingia katika penzi zito na NANJALA (MANZI WA NAIROBI)
MAMA SAER Nimama alie kiuka mila za kimasai na kuzaa na mswahili. Kulingana na mila zao ikapelekea kukataliwa huyo mototo alivyo zaliwa. (SAMER) Sama atalelewa upande wa baba ake na kupata na fasi ya kusoma uku akimsaidia mama yake kwa mambo madogo madogo.
SAITOTI Ni mzee wa mila na mwenye utawala kwenye kabila la kimasai. Kutokana anaamini mila itapelekea kuleta maafa makubwa katika boma yao na. vita vitaanza baada ya mmoja wa wanajamii kuamleta mwanamke wa Kiswahili katika himaya yao. (SAITABAU NA NANJALA) Vita vitakuwa vikali sana adi kusababisha mauwaji ya sirisiri katika jamii yao.
KHALILI Ni kijana anae tambulika kama bubu nikijana mchapakazi alie kuja namanga kwa niaba ya kumpokea mpenzi wake anae toka Nairobi (NANJALA) Kwabaati mbaya watapishana na kutokuonana Baada ya khalili kupoteza simu yake. Khalili atafika namanga na kumuona mwanadada akizubaa na simu atamuibia bila ya kujua anae mwibia ndo mgeni anae mngoja kutoka nairobi “NANJALA”
*MANZI WA NAIROBI* Ni tamthilia ya mapenzi, mila,usaliti, familia na mapambano ya kikazi kipya dhidi ya maamuzi yaliyopangwa na wazee. Ni simulizi inayo onesha wakati mwingine upendo wa kweli unaweza kuleta vita kubwa na chuki.
Burudani haijawahi kuwa rahisi hivi!
Usikose kufuatilia tamthilia hii kali ya Manzi wa Nairobi na vipindi vingine vingi vya kusisimua popote ulipo kupitia Zuku App.
Habari njema kwa wateja wapya wa Zuku: Mnapata MWEZI 1 BURE wa kifurushi cha Zuku Lite pindi unapopakua app ya Zuku leo.
Pakua kupitia simu ya Android.
Pakua kwa ajili ya Android smart TV.